Kenya vs Tanzania? Wakenya Wamzomea Zuchu Kasarani – Lakini Je, Ni Haki?
Автор: MIZUKA MEDIA
Загружено: 2025-09-01
Просмотров: 427337
Описание:
Katika fainali za CHAN 2025 Moi International Stadium Kasarani Nairobi, sakata kubwa siyo uwanjani kati ya Morocco vs Madagascar, bali ni kilichotokea wakati Zuchu kutoka Tanzania alipokuwa akijiandaa kutumbuiza mbele ya maelfu ya mashabiki.
Wakenya walitimiza ahadi yao – badala ya kushangilia, mashabiki wengi walianza kuimba Wimbo wa Taifa la Kenya mara tu Zuchu alipoanza kuimba. Tukio hili limezua mjadala mkali mitandaoni: wengine wakisema Wakenya wamemdhalilisha, wengine wakisema ni haki yao kulinda heshima ya taifa na kupendelea wasanii wa Kenya kama Ssaru, Maandy, Diana Cods na Toxic Lyrically.
Watanzania nao hawakubaki nyuma – baadhi wamesema wamechoshwa na tabia za Wakenya, huku wengine wakidai Zuchu amechanganyikiwa kwa namna alivyopokelewa. Hata hivyo, kuna sauti za busara zikisema ni muhimu jirani kuishi vizuri na jirani, kwani hutajua lini utamhitaji.
Sasa swali kuu ni: Je, Wakenya walifanya haki kwa kumzomea Zuchu Kasarani, au huu ni ushindani wa kawaida wa Kenya na Tanzania? 🇰🇪🇹🇿
👉 Tazama video hii hadi mwisho kupata maoni ya mashabiki wote, kutoka Kenya na Tanzania, na usisahau kusubscribe MIZUKA MEDIA kwa habari zote za mastaa, siasa na maisha ya kila siku.
#Zuchu #CHAN2025 #KenyaVsTanzania #BongoFleva #MIZUKAMEDIA #Kasarani
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: