KIPINDI CHA IJUE TUME YA UTUMISHI WA MAHAKAMA MKOA WA ARUSHA.
Автор: Tume ya Utumishi wa Mahakama (JSC)
Загружено: 2025-10-02
Просмотров: 29
Описание:
Kifungu cha 33 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama sura ya 237 kimeruhusu Tume ya Utumishi wa Mahakama kukasimu majukumu yake kwa kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ambazo zimeainishwa kwenye kifungu cha 36 cha Sheria hiyo. Hata hivyo, kifungu cha 50 cha Sheria hiyo kinaunda Kamati za Maadili ya Maafisa Mahakama ngazi ya Mkoa na ngazi ya Wilaya.
Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Ibara ya 112 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Sheria ya Usimamizi wa Mahakama sura ya 237. Chombo hiki kiliundwa kwa lengo la kusimamia Uendeshaji wa Mahakama ya Tanzania.
Aidha, Mamlaka ya Tume ya Utumishi wa Mahakama kama chombo cha kusimamia ajira na nidhamu za Watumishi wa Mahakama yanatokana na Ibara ya 113 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikisomwa pamoja na kifungu cha 29 (1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mahakama Sura ya 237.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: