MAUMIVU YA SIKIO: Kujitibu mwenyewe nyumbani
Автор: WikiElimu
Загружено: 2025-03-17
Просмотров: 8803
Описание:
Maumivu ya sikio mara nyingi yanasababishwa na kujaa kwa majimaji kwenye sehemu ya kati ya sikio (sehemu iliyo baada tu ya ngoma ya sikio). Katika hali ya kawaida, majimaji yanayotengenezeka kwenye sehemu ya kati ya sikio yanatiririshwa kutoka hapo kwenda kwenye pua kwa mfereji unaoitwa eustachian tube. Ila wakati wa mafua au aleji, tishu ndani ya oua zinavimba na kufunga kabisa mfereji huu; tatizo hili linatokea zaidi kwa watoto kwa sababu mfereji wao bado ni mdogo sana na ni rahisi kuzibika. Kwa sababu mfereji huu umebiza majimaji yanaanza kujaa hapo na kusababisha maumivu na hata kushindwa kusikia vizuri.
Majimaji yaliyotwama yanatoa mazingira mazuri ya bakteria kukua na kusababisha maambukizi. Maambukizi haya yanasababisha maumivu na homa, na mara nyingi inatokea kwenye sikio moja.
Kuna watu pia, wanahisi maumivu na kushindwa kusikia vizuri wapokuwa wanapanda kwenda nyanda za juu, kwa mfano wanaopanda mlima au wanaopanda ndege. Hapa pia mfumo ni ule ule mfereji wa eustachian tube unaziba. Unaweza kufungua mfereji huu kwa kufunga mdomo, ziba pua kwa vidole vyako, kisha jaribu kama unapuliza pua; hii ni njia mojawapo ya kufungua mfereji wa eustachian tube. Unaweza pia kutumia dawa za mafua “decongenstant” kupunguza shuda hii.
Maambukizi ya sikio kwa watoto
Kwa mtoto mwenye maambukizi sikioni atakuwa na dalili kama zifuatazo; homa, maumivu ya sikio, atakuwa hatulii, Analia sana, mchungu sana, na atakuwa anavutavuta sikio lake. Kwa sababu watoto wachanga hawawezi kukuambia kama sikio linauma, akiwa Analia sana na anavuta sikio ni vizuri afike kwa daktari. Kama wewe ni mzazi usiwe na wasiwasi, watoto wengi huwa wanapata shida kusikia kwa muda huo, ila wakipata matibabu wanarudi kuwa kwenye hali ya kawaida kabisa ya kusikia.
Mambo ya kufanya ukiwa nyumbani kama una maumivu ya sikio
Dawa kama Antihistamines, decongestants, na dawa za kudondoshea puani (nose drops) zinasaidia kupunguza majimaji yanayotiririka na kusaidia utandi ute ndani ya pua kusinyaa ili kufungua mfereji wa eustachian tube. Mara nyingi matibabu ya nyumbani tu yanatosha kuondoa majimaji haya kutoka sikioni.
Kutumia dawa kama Acetaminophen, aspirin, ibuprofen, au naproxen zitasaidia kukupunguzia maumivu. Usimpatie mtoto dawa ya Aspirin bila ushauri wa daktari, inaweza kusababisha tatizo hatari linaloitwa Reyes syndrome, tatizo hili linaharibu ubongo na ini.
Unaweza kujifukiza ili kulainisha kamasi na kuongeza mvuke ndani ya pua; chukua bakuli lenye maji ya moto, chukua kitambaa jifunike kichwani kisha inamia bakuli; vuta mvuke – kama hili ni gumu, oga maji ya moto itasaidia pia.
Kama dalili zitaendela kuwepo hata baada ya wiki 2, nenda kaonane na daktari.
Ukifika kwa daktari
Daktari atakuchunguza pia, sikio na koo na ataangalia mfupa ulio nyumba ya sikio “mastoid” – kama ni mwekundu au unauma itamaanisha una maambukizi makali.
https://wikielimu.org/
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: