Heri Kabisa & Yote Ninayo Niliyapokea - Tabernacle Chrétien de Lubumbashi
Автор: Maranatha : Come, O Lord
Загружено: 2022-01-25
Просмотров: 1922
Описание:
Heri Kabisa & Yote Ninayo Niliyapokea - Tabernacle Chrétien de Lubumbashi
Timecodes
00:00 - Heri Kabisa - Nyimbo za Mungu 138
03:34 - Yote Ninayo Niliyapokea - Nyimbo za Mungu 87
HERI KABISA - Nyimbo za Mungu 138
1.
Heri kabisa, Yesu ni wangu!
Ni Muchungaji, na mimi ni wake;
Nimezaliwa mara ya pili,
Ninasafishwa kwa damu yake.
Chorus
[ Yesu ni wimbo wa roho yangu,
Nitamusifu hata milele ] BIS
2.
Kule mbinguni kuna furaha
Ju-u ya mwenye kutubu makosa;
Nilisikia Neno la Mungu,
Nilijitoa kwa Bwana Yesu.
3.
Ninashukuru Yesu Mwokozi,
Na roho yangu inashangilia;
Mimi si kitu mbele ya Mungu,
Kwa neema yake ananipenda.
4.
Ninastarehe sasa kwa Yesu,
Nina salama kutoka kwa Mungu;
Ninangojea Yesu afike
Kunipeleka kwake mbinguni.
YOTE NINAYO NILIYAPOKEA - Nyimbo za Mungu 87
1.
Yote ninayo niliyapokea
kwa wema wake unaoenea;
Mimi si kitu, namutegemea ;
nimeokolewa ka ne-ema.
Chorus
Niliyekuwa nimetoroka,
kwa pendo lake nimeokoka!
[ Yesu ni mwema na mwenye rehema.
Nimeokolewa kwa ne-ema ! ] BIS
2.
Nilitembea zamani kwa zambi
katika njia ya kufa, lakini
Yesu alinitafuta polini ;
nimeokolewa kwa ne-ema.
3.
Nimetakaswa na Yesu Mwokozi,
si kwa matendo na si kwa machozi,
Ila kwa damu nina ukombozi ;
nimeokolewa kwa ne-ema.
4.
Raha ya mbingu imeni-ingia,
kwa shangwe kubwa namufurahia.
Kwa kuwa Yesu ’nanirehemia ;
nimeokolewa kwa ne-ema.
Heri Kabisa & Yote Ninayo Niliyapokea - Tabernacle Chrétien de Lubumbashi
Nyimbo za Mungu 138 & Nyimbo za Mungu 87
#Maranatha
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: