RAIS MWINYI AMEFUNGUA GHALA LA KUHIFADHIA CHAKULA PEMBA UJENZI WA BANDARIZA MKOANI,SHUMBA MJINIWETE
Автор: Tifu Tv
Загружено: 2025-01-08
Просмотров: 4527
Описание:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inajipanga Kutafuta njia Bora za kupunguza gharama za Bidhaa za Chakula kwa Wananchi wa Pemba .
Rais Dk, Mwinyi ametoa tamko hilo alipofungua ghala la Kuhifadhia bidhaa za Chakula Gando , Wilaya ya Wete ,Mkoa wa Kaskazini Pemba linalomilikiwa na Kampuni ya Yasser Provision .
Rais amesema Serikali inalenga Kuwapunguzia Mzigo wa Gharama Wafanyabiashara .wanaoleta bidhaa za Chakula nchini ili kuwepo kwa Unafuu wa bei kwa Wananchi.
Aidha Dk,Mwinyi ameielezea Njia nyengine ni kuwa na Ushuru Maalum kwa Bidhaa zinazopelekwa Pemba .
Dk,Mwinyi amebainisha kuwa Mpango wa kuifungua Pemba Kiuchumi una dhamira thabiti ya kuhakikisha Bei za bidhaa Muhimu zinashuka na kutoa unafuu wa maisha kwa Wananchi.
Amefahamisha kuwa Ujenzi wa Bandari za Mkoani,Shumba Mjini na Wete ambao utaanza karibuni ni miongoni mwa hatua muhimu ya Kuwawezesha Wafanyabishara kuleta Mizigo yao Moja kwa moja Pemba kutoka nchi wanazoagiza ili kupunguza gharama za mzunguko wa Usafirishaji.
Rais Dk ,Mwinyi amepongeza hatua ya Ujenzi wa ghala iliofanywa na Kampuni ya Yasser Provision kuwa ni wa umuhimu utakaosaidia mbali na Hifadhi ya Chakula pia kupungua kwa bei ya bidhaa na kuahidi kwa Serikali Kumuunga Mkono Mfanyabiashara huyo kwa kuhakikisha Mzigo anaoleta Unashushwa Kaskazini Pemba.
Dk, Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inajipanga kwa Ujenzi wa Maghala ya Kuhifadhia Chakula ili kuwa na Uhakika wa Chakula hivyo kujitokeza kwa Sekta binafsi kuanza kujenga ghala ni jambo linalopaswa kuungwa Mkono.
Naye Mmilki wa Ghala hilo Adil Yakoub Sadik lililogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 3.5 lenye Uwezo wa Kuhifadhi Bidhaa mbalimbali bila ya athari yoyote amesema ni mbali na Kuchangia Kodi kwa Serikali pia linatoa thamani ya moja kwa moja ya ajira kwa Wananchi wa Pemba.
Ufunguzi wa ghala hilo ni miongoni mwa Shamrashamra za Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: