UHAMIAJI WACHUKUA HATUA ASKARI WALIOONEKANA WAKIMUADHIBU MTUHUMIWA
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2021-05-30
Просмотров: 89559
Описание:
Idara ya uhamiaji imewasimaisha kazi askari wake watatu kwa tuhuma za kutumia nguvu kinyume cha sheria na maadili ya kazi zao dhidi ya mtuhumiwa wa utapeli Alex Raphael Kyai kama ilivyoonekana katika video fupi iliyosambaa katika mitandao ya kijamii.
Mtuhumiwa huyo anadaiwa kulaghai na kupokea fedha kutoka kwa wateja mbalimbali ili waweze kupata pasipoti kwa haraka pia amekuwa akijitambulisha kama mtumishi wa Taasisi nyeti ikiwemo Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
"Hatua ambazo Idara imechukua dhidi ya askari, tumewasimamisha kazi kupisha uchunguzi wa tukio lenyewe lakini pia mtuhumiwa tumemfikisha kwenye mamlaka husika ili aweze kuendelea na utaratibu mwingine kisheria"-Dkt. Anna Peter Makakala, Kamishina Jenerali wa Uhamiaji.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: