Luxury Home Busted in Sh5 Million Illicit Alcohol Raid, ELDORET
Автор: Across Kenya Media
Загружено: 2026-01-16
Просмотров: 60
Описание:
Polisi wa Kaunti ya Uasin Gishu wamefichua biashara haramu ya pombe iliyokuwa ikiendeshwa ndani ya jumba la kifahari katika eneo la makazi. Makasha ya pombe yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano yalipatikana yakihifadhiwa ndani ya nyumba hiyo, huku mshukiwa mmoja akikamatwa.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti hiyo, Benjamin Mwanthi, amesema pombe hiyo inadaiwa kuwa haramu na haijalipiwa ushuru, hatua inayokiuka sheria. Alisema operesheni hiyo ilifanyika kwa ushirikiano na taasisi za serikali zikiwemo KRA, ACA, KEBS na Bodi ya Kudhibiti Vileo ya Kaunti ya Uasin Gishu.
Mwanthi ameongeza kuwa washukiwa 147 wamekamatwa katika kaunti hiyo kwa kuhusika na biashara ya pombe haramu, wengi wao wakiwa wanaume. Sheria ya Kenya inapiga marufuku uuzaji wa pombe katika maeneo ya makazi na karibu na shule, huku serikali ikiendelea kutekeleza agizo la Rais William Ruto la kupambana vikali na pombe haramu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: