MAAFISA WA ZAMANI WA DOCKERWOKERS WAITAKA SERIKALI KUONGEZA MKATABA WA CAPT RUTO
Автор: Al Shifaa Television Kenya
Загружено: 2026-01-15
Просмотров: 248
Описание:
Sehemu ya maafisa wa zamani wa Chama cha Wafanyakazi wa Bandari, Dockworkers’ Union (DWU), wamejitokeza tena kuisihi serikali kuhuisha mkataba wa Kapteni Ruto unaotarajiwa kukamilika ndani ya robo ya kwanza ya mwaka huu.
Wakiongozwa na Paul Abisa kwa niaba ya jamii ya bandari, maafisa hao wamempongeza Kapteni Ruto kwa mafanikio makubwa aliyopata, ikiwemo kushughulikia tani milioni 2.145 za makontena aina ya twenty-foot equivalent units (TEUs).
Abisa amesema ongezeko hilo ni hatua kubwa ikilinganishwa na miaka ya awali, akisisitiza kuwa mafanikio hayo si takwimu za kawaida bali ni ishara ya maendeleo ya kweli.
Abisa alikuwa akizungumza na wanahabari katika bustani ya High Level, eneo la Mvita, kaunti ya Mombasa.Afisa huyo wa zamani wa DWU ametoa wito kwa serikali kuzingatia rekodi ya utendaji wa Kapteni Ruto na kuhakikisha mkataba wake unahuishwa kwa misingi ya mafanikio aliyoyapata.
Akiandamana na mwenzake wa zamani wa DWU, Wycliffe Baraza, Abisa amekanusha madai kuwa tathmini yao ni ya kihisia, akisema inategemea takwimu na matokeo halisi ya kipindi cha miaka mitatu tangu Kapteni Ruto alipoteuliwa.
Ameeleza kuwa Mkurugenzi Mkuu huyo anaifahamu bandari kwa undani mkubwa kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya KPA kabla ya kuteuliwa kuwa kiongozi mkuu.
Kwa upande wake, Baraza amesema serikali ilipoteza fursa mapema kwa kutomteua Kapteni Ruto katika nafasi hiyo miaka iliyopita.
Amesema Kapteni Ruto ni mfanyakazi bidii anayestahili kuongezewa mkataba wake kabla ya muda wake kukamilika.
Maafisa hao wa zamani wa DWU sasa wanaitaka serikali kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha uongozi wa Kapteni William Ruto unaendelea, wakisema ni muhimu kwa mustakabali na ushindani wa Bandari ya Mombasa katika soko la kimataifa.
#nairobitrendingnews #news #reels #kenya #mombasa #coast
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: