HIZI HAPA SABABU ZA WAKINGA KUSHIKA UCHUMI HAPA TANZANIA
Автор: NJOMBE TV
Загружено: 2023-12-25
Просмотров: 1387
Описание:
EXCLUSIVE:SIRI NZITO NYUMA YA UTAJIRI WA WAKINGA,HAKUNA USHIRIKINA PROF.ILOMO AFUNGUKA A-Z,NAO WARUDI MAKETE MWISHO WA MWAKA
Miongoni mwa watu wanaofahamika kuwa na uchumi hapa nchini ni pamoja na watu wa kabila la Wakinga kutoka wilaya ya Makete kule mkoani Njombe ambao wamejizolea umaarufu mkubwa kwa kumiliki fedha pamoja na majengo makubwa kutokana na biashara zao wanazozifanya kwenye mikoa mbalimbali na kwenye majiji makubwa ikiwemo Jiji la Dar es Salaam katika eneo la Kariakoo.
Wakinga wameendelea kujizolea umaarufu kwa utajiri huku wao wakifanya mambo yao kimya kimya na kupelekea maneno huku watu wengi wakienda mbali na kudai kuwa huenda utajiri wao unatokana na ushirikina kwa kuwa licha ya kuwa na mali lakini hawawezi kujionyesha huku pia wakishindwa hata kurejea katika maeneo yao ya asili na kubaki kwenye majiji wakitafuta mali.
Profesa Phares Ilomo ambaye ni mhadhili wa chuo Kikuu cha Iringa na kueleza mambo mengi ikiwemo siri ya watu wa Makete kufanya vizuri kwenye biashara ambapo pia amefunguka kuhusu Wakinga kuanza kurejea nyumbani na kufanya uwekezaji kutokana na hamasa kubwa inayofanywa na serikali ya wilaya hiyo kwa kushirikiana na Chama cha Maendeleo Makete (MDA)
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: