UGONJWA WA KIFAFA: Sababu, Dalili, Matibabu
Автор: WikiElimu
Загружено: 2026-01-25
Просмотров: 285
Описание:
Katika video hii nimeeelezea kuhusu Ugonjwa wa kifafa
Kifafa (epilepsy) ni ugonjwa wa ubongo unaotokea kama muundo na shughuli za mfumo wa fahamu kwenye ubongo umevurugika. Tunasema kwamba mtu ana ugonjwa wa kifafa kama amepata matukio mawili ya degedege ambayo yametokea kwa siku mbili tofauti bila sababu ya moja kwa moja inayofahamika. Kama mtu amepata degedege baada ya kupigwa kichwani na kitu kizito – hii sio kifafa – kwa sababu chanzo chake tunakifahamu. Kama mtoto anapata degedege na tukipima ana homa kali sana – hatuwezi kusema kuwa na kifafa maana chanzo cha degedege kinafahamika. Ila kama mtu amepata tukio la degedege na tumefanya vipimo vyote bila kuona sababu ya moja kwa moja inayosababisha tukio hilo la degedege – basi tunaweza kusema kuwa ni kifafa. Hii ndio sababu watu wengi wanaamini kuwa ugonjwa wa kifafa unatokana na uchawi – kwa sababu chanzo cha degedege huwa hakifahamiki moja kwa moja.
Dr. Emmanuel Mniko #mniko #wikielimu
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: