Wazazi wenye watoto waliopitiliza uzito waiangukia Serikali
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-01-14
Просмотров: 5814
Описание:
Wakati furaha ya kila mzazi ni kuona mtoto wake akiongezeka kilo kila mwezi kila anapokwenda kliniki hali ni tofauti kwa familia ya Joseph Kalenga na mkewe Vumilia Elisha baada ya watoto wao kuongezeka uzito kupita kawaida.
Familia hiyo yenye watoto wanne, wawili kati yao Imani Joseph (6) na Gloria Joseph (4) wana uzito kuliko umri walionao, hivyo kutishia usalama wa afya yao.
Wakizungumza na Mwananchi wazazi wa watoto hao wanasema kuwa uzito wa watoto wao unawafanya washindwe kucheza na kufanya mambo ambayo watoto wa umri wao wanafanya kila siku ikiwemo michezo.
Mama wa watoto hao, Vumilia anasema mpaka sasa Imani (6) ana uzito wa zaidi ya kilo 70 huku mdogo wake Gloria (4) akiwa na uzito wa zaidi ya kilo 50.
Akizungumzia historia ya watoto hao mama huyo anasema walizaliwa wakiwa na uzito wa kilo 3 lakini walikuwa wanaongezeka uzito mkubwa kila mwezi kati ya kilo tatu hadi nne hali iliyowashtua hata manesi wa kliniki ambao walimshauri kuwanyonyesha kwa ratiba maalum.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: