IDADI ya WALIOFARIKI kwa KUFUKIWA na KIFUSI cha MGODI wa DHAHABU IMEONGEZEKA na KUFIKIA 22
Автор: Global TV Online
Загружено: 2024-01-14
Просмотров: 3946
Описание:
IDADI ya WALIOFARIKI kwa KUFUKIWA na KIFUSI cha MGODI wa DHAHABU IMEONGEZEKA na KUFIKIA 22
Idadi ya watu waliofariki kwa kufukiwa na vifusi katika Mgodi wa dhahabu Ikinabushu Wilayani Bariadi Mkoa wa Simiyu imefikia 22 kutoka 16 waliokuwa wametolewa katika vifusi hivyo hadi Jana jioni.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Faustine Mtitu amesema mpaka Jana majira ya saa 2:00 usiku, jumla ya wachimbaji wadogo wote wanaume 22 walitokewa kwenye mashimo ya Mgodi huo wakiwa tayari wamepoteza maisha.
" Leo Januari 14, 2024 tumekagua mashimo yote ambayo yaliporomoka kwenye Mgodi huu, kujiridhisha kama Kuna mwili ulisalia, na ukaguzi umemalizika na jumejirisha kuwa hakuna mwili uliyobaki, na vifo idadi imefikia 22 kutoka 16," Amesema Mtitu.
Amesema kuwa kazi iliyobaki ni kufukia baadhi ya mashimo ambayo ni hatarishi kwenye Mgodi huo, ambapo ameeleza kuwa kazi hiyo itafanywa na mashine aina ya Skaveta kwa kusimamiwa na Jeshi hilo.
Usiku wa kuamkia Jana Majira ya saa 11, Arfajiri baadhi ya mashimo katika Mgodi huo, yaliporomoka na kuwafukia baadhi ya wachimbaji wadogo ambao walikuwa wakiendelea na zoezi la uchimbaji wa Madini.
============================================================
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 713 750910), ( +255 783453136)
⚫️ Email: [email protected]
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: • Habari zote za michezo na Burudani Tanzania!
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: