KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 17/02/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-02-17
Просмотров: 3473
Описание:
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 17/02/2026
UJUMBE WA LEO: MAMBO YATAKAYOKUWEZESHA KUTOKA NYUMBA YA UTUMWA MPAKA UTIMILIFU WA AHADI
Mithali 22 : 1
1 Nyakati 4 : 9 - 10
Ufunuo 2 : 17
Mwanzo 32 : 28
I Samweli 25 : 25
Mithali 22 : 1
1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.
1 Nyakati 4 : 9 - 10
9 Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.
10 Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.
Ufunuo 2 : 17
17 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Mwanzo 32:28
28 Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.
I Samweli 25 : 25
25 Nakusihi, bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; kwa maana kama lilivyo jina lake ndivyo alivyo yeye; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma.
AGENDA ZA MAOMBI KUFUNGULIWA KUTOKA CHINI YA KITI
1️. OMBA TOBA YA KUJINASUA KUTOKA KWENYE NAFASI YOYOTE INAYOWEZA KUKUSHIKILIA KWA UHALALI WA SADAKA.
2️. OMBA MKONO WA MUNGU KWA NJIA YA SADAKA IMKOMBOE MZALIWA WA KWANZA AU IKUTOE MAHALI ULIPOSHIKILIWA KWA SADAKA YA MADHABAHU YA MIUNGU MINGINE (KWENYE KITI CHA ENZI CHA FARAO)
Mhubiri: Mwl.Renald Mlawi.
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: