UTALIA !! MTOTO WA MIAKA 13 ALIEOKOTWA NA BIBI / BABA NA MAMA YAKE WAFARIKI AOMBA MSAADA
Автор: Families Media
Загружено: 2026-03-14
Просмотров: 111
Описание:
Kijana huyu anaitwa Shabani, mtoto ambaye maisha yake yamegubikwa na changamoto nyingi tangu akiwa mdogo. Shabani anaishi bila baba wala mama, kwani wazazi wake wote walishatangulia mbele za haki. Kwa sasa anaishi na bibi yake ambaye ndiye mlezi wake pekee anayejitahidi kumlea licha ya hali ngumu ya maisha.
Kila siku Shabani huamka mapema sana asubuhi na kuanza pilika pilika za kutafuta riziki mtaani. Cha kusikitisha ni kwamba kazi anayofanya haifanani kabisa na umri wake, lakini analazimika kuifanya ili kusaidia maisha yao na kutimiza ndoto yake kubwa ya kurudi shule.
Ndoto ya Shabani ni kuendelea na masomo, baada ya kufukuzwa shule alipokuwa Kidato cha Pili kutokana na kukosa ada ya shule. Kwa matumaini ya kupata fedha za kurudi darasani, anaendelea kufanya kazi ngumu kila siku. Lakini hali ni ngumu zaidi kwani kuanzia asubuhi hadi jioni, mara nyingi hupata shilingi elfu moja tu, huku akirudi nyumbani akiwa amechoka sana na macho yake kuvimba kutokana na mwanga mkali wa jua.
Familia inayomlea kijana huyu wanasema wana ndoto kubwa ya kumuona Shabani anarudi shule na kutimiza ndoto zake. Hata hivyo, uhaba wa kipato umekuwa kikwazo kikubwa kinachowazuia kufanikisha hilo.
Wahenga wanasema “Kutoa ni moyo na si utajiri, na mkono unaotoa ndio unaopokea.” Ikiwa utaguswa na habari hii ya Shabani, unaweza kuwa sehemu ya kubadilisha maisha yake kwa kumpa msaada ili aweze kurudi shuleni na kujenga mustakabali wake.
NAMBA YA MSAADA NI : 0671823715 ASIA MOHAMEDI ABDALLA
#news #zuchu #matukio #mafuriko #azamtv #millardayo #live #leo
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: