MARIANA AWACHONGEA MADEREVA WA DALADALA KWA WAZIRI MBARAWA
Автор: JUHUDI DIGITAL
Загружено: 2026-02-04
Просмотров: 47
Описание:
Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imetambua changamoto zinazowakabili wanafunzi wanaotumia usafiri wa mabasi ya mijini, hususan daladala, kufuatia barua iliyoandikwa na mwanafunzi Mariana Eric Mirindima wa Shule ya Sekondari Jangwani. Katika barua hiyo, mwanafunzi huyo alieleza vitendo vya baadhi ya madereva na makondakta kugoma kuwabeba wanafunzi kwa madai ya kibiashara, hali inayosababisha wanafunzi kuchelewa au kushindwa kabisa kufika shuleni, kuhatarisha usalama wao na kuathiri haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame M. Mbarawa, amemshukuru mwanafunzi huyo pamoja na mzazi wake kwa ujasiri wa kutoa mrejesho kwa Serikali, akisisitiza kuwa sauti ya wanafunzi imesikilizwa na itafanyiwa kazi. Serikali imesisitiza kuwa, licha ya kutoa fursa kwa sekta binafsi kutoa huduma za usafiri wa umma, watoa huduma hao wanapaswa kuzingatia sheria, kanuni na viwango vya utoaji huduma vinavyosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).
Katika kuboresha usafiri wa wanafunzi mijini, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo kuanzisha mabasi maalumu kwa ajili ya wanafunzi nyakati za asubuhi na jioni, kutenga mabehewa maalumu ya wanafunzi katika treni za mijini, kurasimisha nauli ya Shilingi 200 kwa wanafunzi, pamoja na kusimamia kikamilifu uthibitishaji wa madereva na usajili wa makondakta. Hatua hizi zinalenga kuhakikisha wanafunzi wanapata usafiri salama, wa uhakika na wa gharama nafuu.
Aidha, Waziri ameielekeza LATRA kuimarisha udhibiti wa nauli, kutoa adhabu kali kwa wanaokiuka sheria, kutoa elimu kwa watoa na watumia huduma, pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara. Serikali pia imewataka wananchi kushirikiana kwa kutoa taarifa za ukiukwaji kupitia namba za bure na mitandao ya mawasiliano, huku ikisisitiza umuhimu wa kulinda haki, usalama na ustawi wa wanafunzi katika mfumo wa usafiri wa umma nchini.
#latra#wizarayauchukuzi
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: