UZINDUZI WA MOTO | MHE. BASHIRU | MHE. FARAJI | NDG, SHABANI | WATEMA CHECHE NDANDA JIMBONI
Автор: MUUNGWANA ONE TV
Загружено: 2025-09-20
Просмотров: 128
Описание:
NDANDA: MBONECHE AZINDUA KAMPENI AKIAHIDI KUWAPA KIPAUMBELE VIJANA
Mgombea udiwani kata ya Ndanda kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Bashiru Mboneche, jana Septemba 20, 2025 alizindua rasmi kampeni zake kwa kunadi sera kwa wananchi wa kata hiyo huku akiweka kipaumbele kwenye ajira na vipaji vya vijana.
Akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo, Mboneche alisema changamoto kubwa inayowakabili vijana wa Ndanda ni ukosefu wa ajira na kutothaminiwa kwa vipaji walivyonavyo, jambo aliloahidi kulishughulikia mara atakapopata nafasi ya kuongoza.
“Vijana wa Ndanda wana uwezo na vipaji vikubwa, changamoto imekuwa ni fursa za kuvikuza. Nitahakikisha tunajenga mazingira rafiki ya ajira na kukuza vipaji ili vijana wetu wasalie kuwa nguvukazi muhimu ya maendeleo ya kata hii,” alisema Mboneche.
Mbunge wa jimbo hilo, aliyeshiriki katika uzinduzi huo, alimnadi mgombea huyo kwa wananchi akisema, “Mboneche anatosha, ana uwezo wa kujenga hoja na kutetea maslahi ya wananchi wa Ndanda.”
Kwa upande wao, wananchi wa kata hiyo walieleza kufurahishwa na sera zilizowasilishwa na mgombea huyo, huku wakiahidi kumpa ushirikiano iwapo atachaguliwa, lakini wakamtaka pia kuhakikisha anatekeleza ahadi hizo mara atakapoanza majukumu yake ya udiwani.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: