UTATA WAIBUKA/NDOA YA MBUNGE NA MTOTO WA MBUNGE YAINGIA 'MDUDU'
Автор: MwanaHALISI TV
Загружено: 2021-07-01
Просмотров: 6668
Описание:
Ndoa ya Mbunge wa Korogwe Vijijini, Timotheo Mnzava na mchumba wake, Caroline Pallangyo, ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Arumeru Mashariki, John Pallangyo, imeingia mdudu baada ya kuwekewa pingamizi kanisani.
Ndoa hiyo inayotarajia kufungwa Julai 10 mwaka huu, imewekewa pingamizi na mwanamke anayefahamika kwa jina la Anna, anayedai kuishi naye na kuzaa naye, kabla ya kuamua kufunga ndoa na mwanamke mwingine kwa kificho.
MwanaHALISI TV imezungumza na mwanamke huyo anayeishi Dodoma kikazi, ambaye ni mtumishi wa Serikali, akisema, aliishi na Mnzava kuanzia mwishoni mwa mwaka juzi na kubahatika kupata naye mtoto mmoja wa kike. Na walianza uhusiano walipokutana Tanga alikokwenda kikazi.
Anna anadai kuwa amewasilisha pingamizi hilo katika Kanisani la Kiijili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Mombo mkoani Tanga, ambamo Mnzava anatarajia kufungia ndoa, akilitaka Kanisa lisitishe matangazo ya ndoa hiyo, zikiwa ni siku chache baada ya Kanisa hilo kuanza kutoa matangazo.
🔘JE, NA WEWE UNA HABARI?
🔘WASILIANA NA MwanaHALISI TV ( +255 767 400402),
🔘WhatsApp ( +255 692 318213)
🔘Email: [email protected]
🔘KWA HABARI ZA KILA SIKU: http://mwanahalisionline.com
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: