🛑TIZAMA KWATA LA WAHITIMU JESHI LA AKIBA KUTOKA JAMII YA KIMAASAI🛑
Автор: Smile Media
Загружено: 2025-09-05
Просмотров: 2353
Описание:
Na.Mwandishi wetu
DC LONGIDO AFUNGA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA AKIBA.
Mkuu wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha Salum Kalli leo tarehe 5 Septemba,amefunga rasmi mafunzo ya awali ya Jeshi la akiba wilayani humo.
Akizungumza katika hitimisho hilo kalli,amewataka wahitimu wote kutofanya wala kujaribu katika mitaa mafunzo yote waliyoyapata kipindi cha miezi mitatu bali wapokee maelekezo kutoka kwa wakuu wao.
Aidha kalli,amewapongeza wahitimu wa kike ambao jumla yao ni 8 kwa kufanya vizuri kwani ni wachache wanaweza jitolea kufanya mafunzo hayo yaliyojaa ukakamavu,ujasiri na kujitoa haswa.
Kalli,amewataka wahitimu hao kuwa tayari muda wowote kutumika katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania na hasa katika kipindi hiki ambacho Nchi inaelekea katika zoezi la Uchaguzi Mkuu.
Katika tukio hilo Mkuu huyo wa Wilaya amabae ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ameambatana na wajumbe wa kamati ya usalama na kushuhudia mamia ya wananchi wakijitokeza kwa wingi katika tukio hilo.
@
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: