"VITENDEA KAZI HIVI SIO VYA SHAMBA BINAFSI" – DKT JOHN JINGU
Автор: SINGIDA RS
Загружено: 2026-01-02
Просмотров: 80
Описание:
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John A. K. Jingu, amegawa pikipiki nane (8) kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa kata katika halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Singida, na kuwataka wazitumie kwa kuwafikia walengwa wa miradi ya maendeleo — badala ya kuzitumia kwa shughuli binafsi.
Pikipiki hizo zimekabidhiwa katika hafla iliyofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, kama sehemu ya mpango wa Serikali wa kuboresha utendaji kazi katika ngazi za msingi kupitia Mpango wa “Bottom-Up”.
Akizungumza wakati wa makabidhiano, Dkt. Jingu amesema pikipiki hizo ni miongoni mwa pikipiki 98 zilizonunuliwa na Wizara katika mwaka wa fedha 2024/25, kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa watendaji wa maendeleo ya jamii katika kata na vijiji.
“Lengo kuu ni kuwawezesha Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwafikia wananchi kwa urahisi, hasa walioko maeneo ya vijijini. Ninaelekeza pikipiki hizi zitumike kwa kazi za Serikali pekee, sio kwa matumizi binafsi,” amesema Dkt. Jingu.
Amesema hadi sasa Serikali imegawa jumla ya pikipiki 208 tangu mwaka 2022/23, na pikipiki 80 nyingine zinatarajiwa kugawiwa mwaka 2026 kupitia Mradi wa Pamoja, hatua itakayoongeza nguvu katika kufikia jamii na kusimamia miradi ya maendeleo.
Dkt. Jingu ameongeza kuwa vifaa hivyo vitasaidia kuboresha usimamizi wa shughuli za kiuchumi katika jamii ikiwemo VICOBA, SACCOS na program za ustawi wa makundi maalum, pamoja na kurahisisha ufuatiliaji wa miradi na utoaji wa taarifa.
“Natarajia Maafisa mtazitunza pikipiki hizi, mtazitumia kwa uaminifu na kwa malengo yaliyokusudiwa, ili zisaidie jamii kwa muda mrefu,” amesema.
Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi – Utawala na Rasilimali Watu, Stephen Pancras, ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuimarisha vitendea kazi mkoani Singida, akisema hatua hiyo imeongeza morali na ufanisi kwa watumishi.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Wilaya ya Ikungi, Mariam Abdalah, amesema pikipiki hizo zitapunguza changamoto za usafiri katika kata zenye vijiji vilivyo mbali na kuimarisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
“Awali tulikuwa tunatembea umbali mrefu kufika vijijini, sasa jamii itafikiwa kwa urahisi na kwa wakati,” alisema.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii, viongozi wa halmashauri, pamoja na wadau wa ustawi wa jamii kutoka taasisi mbalimbali.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: