SANAA YA USUSI KWA KUTUMIA MIANZI
Автор: H3G TV
Загружено: 2024-06-10
Просмотров: 330
Описание:
FAIDA YA MIANZI (BAMBOO) KATIKA SANAA.
Mti wa mianzi(Bamboo tree) una faida nyingi sana kama jamii husika hususani wasanii wataamua kuwekeza katika zao hili.
SALUM JUMA SUDI mwenye umri wa miaka 25 kutoka kijiji Kimambila kata ya Lubungo mkoani Morogoro yeye amebobea katika Sanaa ya Ususi kwa kutumia mianzi anasema, licha ya Mti wa Mianzi kutumika katika kutengeneza pombe aina ya Ulanzi kwa watu wa Iringa pia miti huu unatumika pia kwa ujenzi na uezekaji wa nyumba, ususi wa vikapu na nyungo na thamani nyingine nyingi za Sanaa.
Hivyo anaziomba Taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo kwa ushirikiano na Tamisemi kuja na mpango mkakati hasa katika mikoa ya pembezoni mwa Tanzania kuwawezesha vijana kupata mafunzo kuhusu Sanaa inayotumia mianzi kama sehemu ya kutengeneza ajira kwa vijana wengi walio vijijini.
Anasema kwa hivi sasa baadhi ya bidhaa wanazotengeneza kutokana na mianzi ya miti huko Morogoro ni pamoja na matenga ya nyanya, nyungo, vikapu,mabegi ya akina mama, fagio, viti, mikeka, , vitanda, masanduku,mapambo nk.
Aidha, amesema kama vijana wanakabiliwa na changamoto ya elimu na masoko ya uhakika ya bidhaa zao hivyo wanaomba Taasisi husika ikiwemo BASATA kupitia maafisa Utamaduni waendelee kuwasaidia katika kupata mafunzo ili malengo yao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: