SEMINA YA UJASIRIAMALI ST JOSEPH CATHEDRAL (JINSI YA KUJIAJIRI NA KUJIINGIZIA KIPATO KIKUBWA) PART 1
Автор: Kwaya ya Familia Takatifu St. Joseph Cathedral DSM
Загружено: 2019-07-30
Просмотров: 4113
Описание:
Semina hii ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Parokia ya Kanisa kuu la Mtakatifu Yosefu Jimbo kuu la Dar es salaam maalum kabisa kwa VIWAWA na wengine wote wenye uhitaji imelenga kutoa elimu ya masuala ya kiuchumi, ni namna gani kijana unaweza ukatumia fursa ulizonazo kuweza kujiajiri na kutengeneza ajira kwa vijana wengine. Shukrani za pekee ziende kwa Paroko wa kanisa kuu Fr. Dr Joseph Matumaini ambaye ametuandalia Semina hii bila kumsahau mtoa semina wetu Kaka Thomas. Karibuni tuweze kupata mafundisho haya. Mungu awabariki sana.
Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali.
1. Kuwa mtatuzi wa matatizo
Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.
Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.
“Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu”
2. Kuwa na maono
Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.
“Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia”
3. Chagua washirika au timu sahihi
Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.
Soma pia: Makosa 15 Ambayo Kila Mjasiriamali Anatakiwa Kuyaepuka.
4. Toa huduma au bidhaa yenye tija
Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.
Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.
Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.
5. Fahamu na jali wateja
Ikiwa wewe ni mjasiriamali, basi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji wewe. Fahamu kuwa wewe kama mjasiriamali, ndiye unaye wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha mambo haya kuhusu wateja:
Fahamu wanataka nini.
Sikiliza maoni na ushauri wao.
Hakikisha unakamilisha mahitaji yao.
Tumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.
Mfanye mteja aone unamthamini.
Mfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla ya pesa.
Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.
6. Tumia pesa vyema
Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.
Soma pia: Njia 10 Zitakazokuwezesha Kutumia Pesa Vyema.
Ni wazi kuwa matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.
Unaweza pia kujifunza wewe mwenyewe jinsi ya kutunza na kutumia pesa vyema; unaweza pia kutumia programu za bure za kompyuta kama vile Wave app kutunza mahesabu yako.
7. Jifunze kusema hapana
“Hapana” ni jibu dogo lakini lenye manufaa makubwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kusema hapana kwani itakutenga na mambo au mipango isiyokuwa na ulazima.
Kuna watu, mipango, vitu au hata tabia ambazo zinaweza kukuathiri vibaya sana kwenye ujasiriamali wako. Hivyo kusema hapana kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na mambo haya.
Soma pia: Tabia 10 zitakazobadili maisha yako.
.................soma zaidi...............................
https://www.fahamuhili.com/kanuni-za-...
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: