3- Darsa | Kitaabu Sswiyam - AlFiqhul-Muyassar | Ustadh Abdulrashed Alhilaly حفظه الله
Загружено: 2026-02-13
Просмотров: 273
Описание:
Silsila Ya Darsa Za Kitabu cha Swiyām katika Fiqhul Muyassar kwa jumla inaelezea maana ya saumu, hukumu yake, masharti na nguzo zake, mambo yanayobatilisha na yanayoruhusu kuacha saumu, pamoja na hikima na adabu za ibada hii kwa mujibu wa Qur’ani na Sunnah kwa mtindo mwepesi na unaoeleweka.
3- Darsa Ya Tatu | Mwezi wa Ramadhani unathibiti kuingia kwake kwa kuonekana kwa mwezi (hilal) au kwa kukamilika mwezi wa Shaaban siku thelathini. Mtume ﷺ amesema: “Fungeni kwa kuuona na fungueni kwa kuuona, msipouona basi kamilisheni Shaaban siku thelathini.” (Imepokewa na Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim). Ikiwa mwezi umeonekana kwa ushahidi wa mtu mmoja mwadilifu, Ramadhani huanza. Ama kutoka kwa Ramadhani (kuingia Shawwal na siku ya Eid) kunathibiti kwa kuonekana mwezi wa Shawwal au kukamilika Ramadhani siku thelathini, na hapa wanahitajika mashahidi wawili waadilifu.
Kuhusu niyya ya swaumu, ni sharti ya ibada na mahali pake ni moyoni. Kwa swaumu ya faradhi kama Ramadhani, ni lazima mtu awe ameweka nia usiku kabla ya kuchomoza alfajiri. Mtume ﷺ amesema: “Yeyote asiyetia niya kabla ya alfajiri hana swaumu.” (Imepokewa na Sunan Abi Dawud na Jami at-Tirmidhi). Hivyo, mtu akikusudia moyoni kwamba kesho atafunga Ramadhani, basi hiyo inatosha bila ya kuitamka kwa ulimi.
Ama nyudhuru zinazoruhusu kufungua katika Ramadhani, ni kama ugonjwa unaodhuru au kuchelewesha kupona, safari ya kisheria, hedhi na nifasi kwa wanawake, ujauzito au kunyonyesha kwa khofu ya madhara, pamoja na uzee mkubwa au ugonjwa wa kudumu. Mwenyezi Mungu amesema: “Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyingine.” (Qur'an 2:185). Mwenye udhuru wa muda kama ugonjwa au safari atalipa siku alizokosa baada ya Ramadhani, na mwenye udhuru wa kudumu kama uzee mkubwa atalisha masikini kwa kila siku (fidya).
Masjid Ummu Salama Utawala Nairobi 265/08/1447H 13/02/2025M
#شرح_كتاب_الصيام_من_الفقه_الميسر
#Kitabu_swiyyam _alFiqhul_Muyassar Ustadh_Abdulrashed_alhilaly
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: