SUZA KILIMANI WAPIGA HODI ZBC NA SHIRIKA LA MAGAZETI KUJIFUNZA UANDISHI WA HABARI KWA VITENDO
Автор: SHUKURU MEDIA
Загружено: 2026-02-22
Просмотров: 89
Описание:
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA) kampasi ya Kilimani wamefanya ziara ya kitaaluma katika vyombo vya habari ikiwemo Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) pamoja na Shirika la Magazeti ya Serikali, kwa lengo la kujifunza kwa vitendo namna ya utayarishaji wa habari, uhariri wa maudhui, uendeshaji wa vipindi pamoja na uchapishaji wa magazeti.
Ziara hiyo imewapa wanafunzi fursa ya kuona kwa karibu mazingira halisi ya kazi za uandishi wa habari, kuhoji wataalamu waliobobea, na kupata uzoefu wa moja kwa moja kuhusu mchakato wa kukusanya, kuandaa na kusambaza taarifa kwa umma.
Hatua hiyo inaonesha dhamira ya SUZA katika kuwaandaa wanahabari chipukizi wenye weledi, maadili na uwezo wa kukidhi mahitaji ya tasnia ya habari ndani na nje ya nchi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: