WATUMISHI 321 AMBAO NI AJIRA MPYA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI WAPEWA MAFUNZO.
Автор: Faida Online TV
Загружено: 2026-02-10
Просмотров: 122
Описание:
Watumishi 321 ambao ni ajira mpya kuanzia January 2025 hadi February 2026 wamepatiwa mafunzo kwa lengo la kuwawezesha watumishi hao kuelewa utumishi wa umma, misingi yake, sheria, kanuni na taratibu za utendaji kazi.
Akizungumza katika hafla hiyo mgeni rasmi Bi Somwana Salumu Manjenga ambaye ni naibu katibu wa sektratarieti ya aajira amewataka watumishi hao kutoa huduma bora na kuwatumikia wananchi kwa uadilifu wa hali ya juu pamoja na uwajibikaji na weledi.
Kwa upande wake mstahiki meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani ametoa wito kwa watumishi hao kuzingatia mafunzo hayo ili wafanye kazi kwa tija katika jamii.
Naye mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Mwl. Hassan Nyange amewahakikishia watumishi hao fedha zao za kujikimu pamoja na masilahi yao huku akiahidi kulipa madeni ya watumishi.
Kwa upande wake katibu tawala wa wilaya ya Mtwara wakili Richard Mwalingo amesema mafunzo hayo ndo msingi wa kazi, huku akiwataka kuzingatia miiko ya kazi ikiwemo utoaji wa huduma bora pamoja na utii kwa serikali na viongozi pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa malalamiko.
SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA HABARI ZETU
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: