Prof. SHEMDOE, BAADA YA KUAPISWA AFANYA KIKAO NA WAKUU WA TASISI ZILIZOPO CHINI YA WIZARA YAKE.
Автор: Uhondo TV
Загружено: 2020-02-03
Просмотров: 708
Описание:
03.02.2020
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemwapisha Katibu Mkuu wa wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe leo Ikulu Dar es Salaam.
Baada ya Kuapishwa Prof. Shemdoe amekutana na watendaji wa Taasisi na Wakala waliochini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Shemdoe amesema kuwa;
“Namshukuru Mwenyezi MUNGU na Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kuniamini na kuniteua kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo imebeba dhima ya nchi kuwa na uchumi wa Viwanda. Nawashukuru wakuu wa Taasisi/Wakala na viongozi wote kwa kufika kuonana nami, ninachotaka kuwasisitiza ni kuwa Tufanye kazi ili kwenda na kasi ya Mhe. Rais wetu ambayo ni kuwa na Tanzania ya Viwanda, tujue kuwa tumepewa jukumu kubwa sana hivyo yatupaswa kushirikiana ili kuyafikia malengo ya Mhe. Rais ambayo anategemea katika Wizara yetu tuyafanye''.
Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo Dkt. Manege Ludovick kwa niaba ya Maafisa Watendaji Wakuu amemshukuru Katibu Mkuu Mteule Prof. Shemdoe kwa na kumuahidi kumpa ushirikiano “ wewe ni Kiongozi wetu tunakuahidi kukupa ushirikiano ili kufikia malengo ya Wizara na nchi kwa ujumla ya kuwa na Tanzania ya viwanda.
Prof. Shemdoe kabla ya uteuzi huu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: