MATUMIZI YA KIAMBISHI KI 1682689005
Автор: MUKUZI KELVIN MWALIMU
Загружено: 2022-03-13
Просмотров: 2137
Описание:
Matumizi ya “Ki-”
Kiambishi Ki - hutumiwa kwa njia mbalimbali: kwa mfano
1. Ki – ya kiwakilishi
Ki- ya kiwakilishi hutumiwa kuwakilisha jina au nomino katika ngeli ya KI – VI hali ya umoja .
Kwa mfano:
i. Mwanafunzi alikichukua kitabu.
ii. Kikulacho ki nguoni mwako.
iii. Kitabu ki mkobani.
iv. Kitumbua alichopika kilikuwa kitamu.
2. Ki – ya masharti
Ki- ya masharti hutumiwa kuonyesha shuruti au lazima.
Kiambishi ki- cha masharti huonyesha kitendo cha kwanza ni lazima kifanyike ili cha pili kitendeke.
Mathalan:
i. Nikiitwa nitaitika. – ni lazima niitwe ili niitike.
ii. Mkila lishe bora mtakuwa na afya bora. – ni lazima mle lishe bora ili muwe na afya bora.
iii. Ukisoma kwa bidii utafaulu masomoni. - Lazima/sharti usome kwa bidii ili ufue dafu.
3. Ki – ya udogo
Ki- ya udogo hutumiwa kuonyesha kukidharau kitu, kudunisha au udogo.
Nomino zote zilizo katika hali ya udogo huandikwa kwa ki- ya udogo.
Mathalan:
i. Mbwa – kijibwa
ii. Karatasi – kijikaratasi
iii. Ndege – kidege
iv. Saa – kijisaa
v. Uso – kijuso
vi. Mbuzi – kibuzi
vii. Mlango - kilango
4. Ki – ya ngeli
ki- ya ngeli hutumika katika viarifu vya ngeli ya KI-VI hali ya umoja
Kwa mfano:
i. Kitabu asomacho kinapendeza.
ii. Kitanda kimenunuliwa.
iii. Kinu kimechongwa vizuri.
iv. Chakula bora kimeandaliwa.
5. Ki – ya namna au kielezi
Ki- ya namna au kielezi hutumika kuonyesha jinsi kitendo kilivyofanyika au kutendeka.
Kiambishi hiki huchukua nafasi ya kama na hivyo kuwa kielezi cha namna.
Ki- hii huwekwa mwanzoni mwa baadhi ya nomino na kuzifanya ziwe vielezi.
Pia huitwa ki- ya kifananisho. Kwa mfano:
i. Wanatembea kama shujaa. - Wanatembea kishujaa.
ii. Anafanya mambo kama mtoto. -Anafanya mambo kitoto.
6. Ki – ya wakati au kuendelea
Ki- ya wakati au kuendelea hutumiwa kitendo katika sentensi kilikuwa kikiendelea wakati huo.
Kwa mfano:
i. Mwenyeji alikuwa akipika pilau mgeni alipowasili.(wakati uliopita)
ii. Mwenyeji atakuwa akipika pilau mgeni atakapowasili. (wakati ujao)
iii. Mwenyeji amekuwa akipika pilau mgeni amewasili. (wakati timilifu)
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: