MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA NUNGWI WAWAPONGEZA WANAFUNZI 74 KWA ZAWADI YA FEDHA TASLIMU
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-01-11
Просмотров: 231
Описание:
Katika muendelezo wa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Nungwi wametoa zawadi ya fedha taslimu kwa wanafunzi 74 waliofanya vizuri katika Mitihani ya Darasa la Saba na kufanikiwa kuchaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari mchipuo.
Hafla hiyo imefanyika katika Skuli ya Kidoti, Mkoa wa Kaskazini Unguja, ambapo zawadi hizo zimetolewa kama ishara ya pongezi za dhati pamoja na lengo la kuwahamasisha wanafunzi hao kuendelea kufanya vizuri zaidi katika masomo na mitihani yao ijayo.
Akizungumza katika hafla hiyo, viongozi hao wameeleza kuwa hatua hiyo inalenga kuhamasisha ushindani chanya miongoni mwa wanafunzi na kuimarisha sekta ya elimu, ambayo ni nguzo muhimu ya maendeleo ya taifa.
Kwa upande wao, wanafunzi waliopokea zawadi hizo wametoa shukrani zao za dhati kwa viongozi hao, sambamba na kutoa ahadi kwa viongozi, walimu na wazazi wao kuwa wataendelea kujituma na kufanya vizuri katika masomo yao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: