MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI TUNDURU: WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KUINGILIA KATI
Автор: Site Tv Online
Загружено: 2026-03-09
Просмотров: 134
Описание:
Wananchi wa Tarafa ya Nalasi, iliyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma wameiomba Serikali kuingilia kati na kutafuta suluhisho la kudumu la migogoro inayojitokeza kati ya wakulima na wafugaji katika eneo hilo ambapo wananchi hao wamependekeza Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutenga rasmi maeneo ya ufugaji ili kudumisha amani na kupunguza migogoro inayotokana na mwingiliano wa shughuli za kilimo na ufugaji.
Wakizungumza mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. BASHIRU ALY KAKURWA, wananchi wamesema kuwa shughuli kuu ya wakazi wengi wa Wilaya ya Tunduru ni kilimo. Hata hivyo, katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na ongezeko la mifugo kuingia katika maeneo ya mashamba, hali inayosababisha migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.
Wananchi hao wamesema migogoro hiyo imekuwa na athari kubwa ikiwemo uharibifu wa mazao, majeruhi na wakati mwingine vifo vinavyotokana na vurugu zinazotokea wakati wa migogoro hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali AHMED ABBAS AHMED, akitoa taarifa kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, amesema Serikali katika Wilaya ya Tunduru tayari imetenga vitalu 279 kwa ajili ya wafugaji. Hata hivyo, amebainisha kuwa maeneo hayo bado hayajapatiwa huduma muhimu kama maji na miundombinu mingine, hali inayowalazimu baadhi ya wafugaji kuyahama na kuingia katika maeneo ya wakulima.
Naye Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt.BASHIRU ALY KAKURWA, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, TAMISEMI pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea na mikakati ya kupanga na kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wafugaji ambayo yatakuwa na huduma muhimu ili kuwezesha wafugaji na mifugo yao kuishi na kufanya shughuli zao kwa utulivu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: