Makongoro Nyerere alivyomvunja mbavu Rais Samia akipewa Tuzo ya kiongozi mchekeshaji
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-02-22
Просмотров: 56939
Описание:
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere ameshinda tuzo ya kiongozi mchekeshaji Tanzania.
Makongoro ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ametwa tuzo hiyo usiku wa leo Jumamosi, Februari 22, 2024 katika kilele cha tuzo za sanaa Tanzania.
Mgeni rasmi kwenye utoaji wa tuzo hizo jijini Dar es Salaam ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.
Katika kipengele hicho, Makongoro alikuwa anashindana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, Mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Richard Hananja na Naibu Waziri na Mkuu wa Mkoa Mstaafu, Aggrey Mwanri.
Mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Makongoro amesema:"Hatimaye, hatimayeee, hatimayeeeee leo nimepata tuzo yangu mwenyewe."
Amesema amekuwa anapokea tuzo ndani na nje nchi za Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na leo amepokea ya kwake mwenyewe. Amewashukuru waandaaji kwa kutambua uwezo wake wa kuchekesha watu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: