Bariadi DC yaadhimisha Siku ya Afya ya Mazingira
Автор: Bariadi DC
Загружено: 2025-09-27
Просмотров: 34
Описание:
Bariadi DC yafanya maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mazingira kwa kutoa elimu na kugawa vifaa mbalimbali vya usafi na utunzaji wa mazingira kama vile vidonge vya kutibu maji, mifuko maalum ya kutibu maji (sawa bag) na uuzaji wa vyoo sungura kwa bei ya punguzo.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kijiji cha Gambosi kata ya Gambosi ambapo wataalamu mbalimbali wa afya kutoka Halmashauri na Mkoa wa Simiyu walihudhuria na kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia kanuni za usafi wa mazingira moja ya faida ikiwa ni kujikinga na magonjwa ya mlipuko kama vile kipindupindu na kuhara.
Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mazingira Duniani mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo "Tokomeza taka za plastiki, Jenga Jamii yenye Afya Bora".
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: