Kanisa Au Siasa? Gen Z Wamshambulia Kiengei Baada Ya Kumkaribisha Ruto
Автор: MIZUKA MEDIA
Загружено: 2026-02-23
Просмотров: 7201
Описание:
Je, Kanisa linapaswa kubaki neutral au lina haki ya kupokea viongozi wa kisiasa? Hili ndilo swali kubwa linalotikisa Kenya baada ya Bishop Ben Kiengei (Muthee Kiengei) wa Jesus Christ Compassion Ministry kumkaribisha Rais William Ruto katika maadhimisho ya miaka 3 ya kanisa hilo, Ruiru – Kiambu County.
Ziara hiyo imezua mjadala mkali mtandaoni, hasa miongoni mwa Gen Z wa Kenya ambao wamekuwa mstari wa mbele katika maandamano ya kupinga serikali tangu sakata la Finance Bill 2024. Baadhi yao wanahisi kuwa Kanisa limegeuka kuwa jukwaa la siasa, huku wengine wakisema Bishop Kiengei alitumia nafasi hiyo kumkumbusha Rais kuhusu ajira za vijana, uwajibikaji wa serikali na haki za Gen Z.
Katika video hii ya uchambuzi, nimekusogezea:
Video za Gen Z wakimshutumu Bishop kwa “usaliti”
Kauli ya awali ya Bishop kuhusu “kutokula na muuaji”
Ahadi ya Rais kwa vijana
Mchango wa kifedha unaodaiwa kutolewa kanisani
Na upande wa utetezi wa Bishop Kiengei
Je, huu ni usaliti kwa vijana?
Je, ni diplomasia ya kiroho?
Au ni mjadala mkubwa wa “Church and State” unaoibuka upya Afrika Mashariki?
Tazama hadi mwisho, sikiliza pande zote, kisha andika maoni yako.
Karibu MIZUKA MEDIA – mahali pa uchambuzi wa siasa, mastaa, na lifestyle ya Afrika Mashariki.
#GenZKenya
#BishopKiengei
#WilliamRuto
#SiasaKenya
#MIZUKAMEDIA
#TrendingKenya
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: