"NILIMWAMBIA MAFURU WEWE NDIO RAIS" RAIS SAMIA AELEZA KWA UCHUNGU ALIVYOFANYA KAZI NA MAFURU
Автор: Gilly Bonny Tv
Загружено: 2024-11-14
Просмотров: 1638
Описание:
"NILIMWAMBIA MAFURU WEWE NDIO RAIS" RAIS SAMIA AELEZA KWA UCHUNGU ALIVYOFANYA KAZI NA MAFURU
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Lawrence Mafuru aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango alikuwa zawadi kwa familia, jamii na hata Taifa, kwani alikuwa mtendaji wa kipekee katika kazi zake.
Rais Samia amesema hayo mkoani Dar es Salaam leo Novemba 14, 2024, alipokuwa akitoa salamu za pole kwa familia na waombolezaji wengine katika Viwanja vya Karimjee, ilipofanyika shughuli ya kuaga mwili wa Lawrence Mafuru.
Amesema Lawrence Mafuru ni mmoja wa mashujaa wa Taifa na mchango wake umeonekana kwa umahiri katika kazi zake, ambapo ameacha alama chanya katika kila sekta aliyofanya kazi.
Rais Samia amewaeleza waombolezaji kuwa aliwahi kumueleza Mafuru wakati wa uhai wake kuwa anafurahishwa na utendaji wake wa kazi hasa katika kushauri kwenye kutatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zinalikumba Taifa.
Rais Samia ameongoza waombolezaji mbalimbali kuaga mwili wa Mafuru aliyefariki dunia Novemba 09, 2024 nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.
Mafuru atazikwa kesho Novemba 15, 2024 katika makaburi ya Kondo, Ununio mkoani Dar es Salaam.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: