ALIYEMUUA MKEWE NA KUMCHOMA NA MAGUNIA YA MKAA AHUKUMIWA KUNYONGWA
Автор: Geah Habibu
Загружено: 2025-02-27
Просмотров: 61012
Описание:
Khamis Luwoga (45) Maarufu kama Meshack aliyekuwa akikabiliwa na shtaka la kumuua mke wake, Naomi Marijani na kisha kuuchoma mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Hukumu hiyo imesomwa jana Februari 26,2025 na Jaji Hamidu Mwanga Wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi 14 wa upande wa Jamuhuri ambao wameweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa mtuhumiwa ametenda kosa hilo.
Na ndugu wa marehemu sasa watakabidhiwa mabaki ya mwili wa ndugu yao kwa ajili ya kwenda kukamilisha taratibu za maziko nyumbani kwao Kilimanjaro.
Ikumbukwe bwana Meshack alifunga ndoa ya kanisani na mkewe Naomi na walibahatika kupata mtoto mmoja wa kike na kisa cha mauaji hayo kwa mujibu wa bwana Meshack ni wivu wa kimapenzi na ni baada ya kukosa maelewano ya muda mrefu na mkewe huyo ,Na siku ya tukio bwana Meshack anasema alimpiga mkewe na alipopoteza maisha alimkatakata kisha akachimba shimo ambalo alikoleza mkaa na kuanza kumchoma kidogokidogo mpaka akamaliza mwili wote na hatimae akabeba mabaki ya mwili huo na kwenda kuufukia shambani kwake mkuranga na kupanda mgomba juu ya shimo hilo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: