Inasikitisha: Hali Halisi ya Mbowe, Ester Matiko Mahakamani.....
Автор: Global TV Online
Загружено: 2019-02-13
Просмотров: 11136
Описание:
Inasikitisha: Hali Halisi ya Mbowe, Ester Matiko Mahakamani.....
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepiga kalenda kesi ya uchochezi inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na wenzake.
Kesi hiyo ilikuwa inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye aliteuliwa kuwa Jaji, ilitajwa leo mbele ya Hakimu Mfawidhi, Kevin Mhina.
Shauri la kesi hiyo limeitishwa kwa ajili ya kutajwa na bado linasubiria rufaa maalum ambayo bado haijasikilizwa.
Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 28, 2019 kwa ajili ya kutajwa na hakimu ameeleza kuwa itapangiwa hakimu mara baada ya rufaa kusikilizwa.
Washtakiwa wengine ni mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko, mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, Katibu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya na Katibu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu.
Wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya FebruarivMosi na 16, mwaka jana maeneo ya Dar es Salaam.
https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website: www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram:
www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jDyho
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: