Mgomo wa Madereva Bolt Watikisa Dar, Wazingira ofisi: 'Wanatunyonya Sana'
Автор: The Chanzo
Загружено: 2024-10-15
Просмотров: 3302
Описание:
Mgomo wa Madereva Bolt Watikisa Dar, Wazingira ofisi: 'Wanatunyonya Sana'
Madereva wa taksi za mtandaoni za kampuni ya Bolt leo Oktoba 15, 2024, wameandamana mpaka makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Morocco, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Madereva hao wanapinga kiwango cha bei za nauli kuwa chini, wanataka makato ya kamisheni yashuke kutoka asilimia takribani 25 hadi asilimia 10, suala la huduma kwa wateja pia wanashinikiza liboreshwe, wanataka abiria nao wawajibike kwenye masuala mbalimbali na pia wanapinga suala la akaunti zao kuzuiliwa ovyo.
Baada ya kufika katika ofisi hizo polisi waliwashinikiza waelekee katika viwanja vya Polisi Oysterbay, kitu ambacho walikubali na baada ya kufika hapo, mkuu wa wilaya ya Ubungo, Saad Mtamule, pamoja na Mkurugenzi wa Bolt, Dimmy Kanyankole, wakafika na kuzungumza nao.
Unaweza kutufuatilia kupitia;
TWITTER: / thechanzo
INSTAGRAM: / thechanzo
FACEBOOK: / thechanzo
TIKTOK: https://www.tiktok.com/@thechanzo?is_...
Au tembelea tovuti yetu: https://www.thechanzo.com
Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo Initiative, 2024 © All Rights Reserved.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: