ycliper

Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
Скачать

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 03/03/2026

Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH

Загружено: 2026-03-04

Просмотров: 3966

Описание: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 03/03/2026

MAFUNGO YA KWARESMA 2026 - SIKU YA 12

NENO KUU:
Mhubiri 3:1
Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Matendo 3:19
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;

MADA:
"KUTOKA MISIMU MPAKA KUSUDI" (FROM SEASONS TO REASON)

UJUMBE WA LEO :
UPAKO WA MAANDALIZI KATIKA MISIMU

SHABAHA:
1. Kujua kwamba kuna upako maalumu wa kimaandalizi katika kila msimu wa maisha, na upako huo unalenga kukusaidia na kukuandaa ili uvuke salama na kufikia kusudi.
2. Kupokea upako unaoachiliwa katika msimu uliopo na faida zake.

1 Samweli 16 : 1, 13
1 Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.

13 Ndipo Samweli akaitwaa pembe yenye mafuta, akamtia mafuta kati ya ndugu zake; na roho ya Bwana ikamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku ile. Basi Samweli akaondoka, akaenda zake Rama.

Zaburi 78 : 70 - 71

70 Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo.

71 Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.

Matendo 13 : 36

36 Kwa maana Daudi, akiisha kulitumikia shauri la Mungu katika kizazi chake, alilala, akawekwa pamoja na baba zake, akaona uharibifu.

1. UPAKO WA MAANDALIZI JUU YA DAUDI NA MISIMU ALIYOPITIA.

Zaburi 89 : 20 - 23

20 Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu.

21 Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu.

22 Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa.

23 Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia.

Matendo 1 : 8

8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

KAZI ZA UPAKO WA KATIKA MISIMU

2. KUKUINULIA WATU WA MSAADA.

1 Samweli 18 : 1 - 5
1 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.

2 Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake.

3 Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.

4 Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.

5 Basi Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia.

1 Nyakati 12 : 1, 21 - 22
1 Basi hawa ndio wale waliomjia Daudi huko Siklagi, alipokuwa akijificha kwa ajili ya Sauli, mwana wa Kishi; nao walikuwamo miongoni mwa wale mashujaa, waliomsaidia vitani.

21 Wakamsaidia Daudi juu ya kile kikosi kilichomshambulia; kwani walikuwa waume mashujaa wote, nao wakawa maakida jeshini.

22 Maana siku kwa siku humjia Daudi watu wa kumsaidia, hata wakapata kuwa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

Wagalatia 2 : 9
9 tena walipokwisha kuijua ile neema niliyopewa; Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika; ili sisi tuende kwa Mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;

AGENDA ZA MAOMBI
1. Omba Mungu akupe upako wa kukuandaa na kukuvusha msimu uliopo ili ufikie kusudi.
2. Omba Mungu akupe upako utakaokutambulisha kwa wengine ili upate msaada kwenye msimu uliopo.

Mhubiri : Mwl. Benjamin Abel.

Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dkt. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]

Не удается загрузить Youtube-плеер. Проверьте блокировку Youtube в вашей сети.
Повторяем попытку...
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 03/03/2026

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио

Похожие видео

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 04/03/2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 04/03/2026

TENZI ZA ROHONI - DEEP RELAX SWAHILI WORSHIP SONGS

TENZI ZA ROHONI - DEEP RELAX SWAHILI WORSHIP SONGS

Understanding and Overcoming Spiritual Resistance || Pastor Peter Mbuguah

Understanding and Overcoming Spiritual Resistance || Pastor Peter Mbuguah

Neema Gospel Choir - Umenibamba (Live Music Video)

Neema Gospel Choir - Umenibamba (Live Music Video)

IRAN YADHIBITI MFEREJI WOTE WA HORMUZ, TRUMP AAPA KUTUMIA JESHI KUPITISHA MELI

IRAN YADHIBITI MFEREJI WOTE WA HORMUZ, TRUMP AAPA KUTUMIA JESHI KUPITISHA MELI

Mch Moses Magembe - KITABU CHA WAEBRANIA

Mch Moses Magembe - KITABU CHA WAEBRANIA

ASKOFU GWAJIMA:KWANINI WATU WA MUNGU WANAONEKANA NI HAWANA MAFANIKIO? LICHA YA AHADI!

ASKOFU GWAJIMA:KWANINI WATU WA MUNGU WANAONEKANA NI HAWANA MAFANIKIO? LICHA YA AHADI!

OMBI LANGU BWANA WANGU 🔥 | 2 Hour Deep Worship & Prayer | Swahili Gospel Mix

OMBI LANGU BWANA WANGU 🔥 | 2 Hour Deep Worship & Prayer | Swahili Gospel Mix

MISIMU & KUSUDI KATIKA MAISHA YA IBRAHIMU (ABRAHAM'S SEASONS & REASON) / REV. DR. ELIONA KIMARO

MISIMU & KUSUDI KATIKA MAISHA YA IBRAHIMU (ABRAHAM'S SEASONS & REASON) / REV. DR. ELIONA KIMARO

JINSI YA KUSHINDA UVIVU WA KUOMBA - Innocent Morris

JINSI YA KUSHINDA UVIVU WA KUOMBA - Innocent Morris

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 03/03/2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 03/03/2026

Nyimbo za Kuabudu na Maombi / Swahili Worship Songs 2 hours of Prayers and Worship GOD

Nyimbo za Kuabudu na Maombi / Swahili Worship Songs 2 hours of Prayers and Worship GOD

NGUVU YA KIBALI  - PASTOR SUNBELLA KYANDO

NGUVU YA KIBALI - PASTOR SUNBELLA KYANDO

Mch Moses Magembe - MPINGA KRISTO

Mch Moses Magembe - MPINGA KRISTO

Ibada ya Lunch hour |  04- 03- 2026 | Mt. Israel Mmary

Ibada ya Lunch hour | 04- 03- 2026 | Mt. Israel Mmary

#LIVE | MISA YA MAZISHI YA PADRE PETER ASSENGA, CSSp (1958 _ 2026) JIMBO KUU KATOLIKI LA ARUSHA

#LIVE | MISA YA MAZISHI YA PADRE PETER ASSENGA, CSSp (1958 _ 2026) JIMBO KUU KATOLIKI LA ARUSHA

OMBI LANGU BWANA WANGU 🔥 | Usiku wa Maombi & Kuabudu (7HRS) | Swahili Gospel Nonstop 2026

OMBI LANGU BWANA WANGU 🔥 | Usiku wa Maombi & Kuabudu (7HRS) | Swahili Gospel Nonstop 2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH :  IBADA YA JUMAPILI - KUSIFU NA KUABUDU 01/03/2026

KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA JUMAPILI - KUSIFU NA KUABUDU 01/03/2026

KUFUTA KALENDA YA MATUKIO YA HASARA - DAY 3 I Jumatano Mchana 04 March 2026

KUFUTA KALENDA YA MATUKIO YA HASARA - DAY 3 I Jumatano Mchana 04 March 2026

JINSI YA KUFUNGA MFUNGO SAHIHI KIBIBLIA - Innocent Morris

JINSI YA KUFUNGA MFUNGO SAHIHI KIBIBLIA - Innocent Morris

© 2025 ycliper. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]