AJALI Mbaya ILIVYOUA Leo Ruvuma, MASHUHUDA Wasimulia A-Z!
Автор: Global TV Online
Загружено: 2019-05-22
Просмотров: 15656
Описание:
AJALI Mbaya ILIVYOUA Leo Ruvuma, MASHUHUDA Wasimulia A-Z!
Watu wawili wamefariki papo hapo na mwingine mmoja kujeruhiwa katika ajali ya gari aina ya lori lenye namba za usajili T 740 DPY lenye tela namba T 427 DGS ambalo mali ya kampuni ya Mohamed Enterpricess ambayo imetokea katika kijiji Kigonsera kilichopo katika wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Akizungumza eneo la tukio mkaguzi msaidizi wa jeshi la zimamoto na ukoaji wilaya ya Mbinga, Jackson Mahali, amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari kufeli breki iliyopelekea kuacha njia na kupinduka ambapo amewataja waliopoteza maisha ni dereva wa gari hilo Sultan Mbwana na mfanyabiashara wa mbao Saleh Ally huku utingo wa gari hilo Omary Kalunde akipata majeraha na kukimbizwa katika zahanati ya Kigonsera.
Naye mmoja wa mashuhuda ambaye ameshuhudia ajali hiyo amesema aliona gari hilo likiwa katika mwendo usio wa kawaida hivyo akaamua kufuatilia ili kuona mwisho wake.
Gari hilo ambalo lilikuwa likitokea Mbinga kuelekea Dar Es Salaam lilikuwa limebeba shehena ya Mbao mali ya mfanyabiashara Saleh Ally ambaye ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
#AJALI
Https://www.youtube.com/watch?v=N1X-f... Watch More Videos here: https://goo.gl/GvVdZw Watch More Videos here: https://goo.gl/ae33fL Website:
www.globalpublishers.co.tz FaceBook: www.facebook.com/globalpublishers Instagram: www.instagram.com/globalpublishers Twitter: www.twitter.com/GlobalHabari Install Global App: ANDROID: https://goo.gl/QvT6RV Install Global App: iOS: https://goo.gl/2jD
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: