MAAGIZO MAZITO: RC MRINDOKO APIGA STOP UKIUKAJI SHERIA ZA ARDHI
Автор: MM MEDIA OFFICIAL
Загружено: 2026-02-24
Просмотров: 84
Описание:
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko amewaagiza watendaji wa Serikali kuzingatia sheria kwa ukamilifu katika uwekezaji, akisisitiza kuwa ukiukaji wa taratibu za ardhi utachukuliwa hatua stahiki mara moja.
Kauli hiyo imetolewa Februari 23, 2026, katika kikao maalum kilichowakutanisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Taasisi na Wakuu wa Idara na Vitengo, huku RC Mrindoko akisisitiza kuanzishwa kwa madawati ya uwekezaji ili kurahisisha utoaji wa huduma na kuongeza uwazi kwa wawekezaji.
Kikao hicho kililenga kujenga uelewa wa pamoja juu ya tafsiri na utekelezaji wa sheria zinazohusiana na uwekezaji. Ambapo RC Mrindoko amezipongeza Halmashauri na taasisi kwa kuendelea kusimamia masuala ya uwekezaji, akibainisha kuwa juhudi hizo zimechangia kuvutia wawekezaji na kukuza uchumi wa mkoa.
RC amesisitiza Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi zinazohusika na masuala ya ardhi kuzingatia kikamilifu sheria na taratibu za umilikishaji wa ardhi kwa wawekezaji. Amesema lipo Tangazo la Serikali linalozuia utekelezaji wa shughuli takribani 15 kwa wawekezaji wasiokuwa raia wa Tanzania, lakini tangazo hilo halifuatiwi.
“Sheria za uwekezaji na ardhi ni lazima zizingatiwe kikamilifu. Hakuna mtu atakayeruhusiwa kuvunja taratibu zilizowekwa. Mwekezaji yeyote asiye raia wa Tanzania anayejihusisha na shughuli zilizozuiwa kisheria hatua zake zichukuliwe mara moja. Huu ni wajibu wetu kulinda maslahi ya Taifa,” alisema RC Mrindoko.
Vilevile, RC amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kufanya tathmini ya miradi yote ya maendeleo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia mwaka 2026 kurudi nyuma. Tathmini hiyo inalenga kubaini matumizi ya fedha zilizowekwa kwa miradi, kuona iwapo miradi imekamilika na kuanza kutoa huduma, na kubaini changamoto zilizopo ili kuzitatua.
Aidha, RC Mrindoko alisisitiza utaratibu wa usafi kwa mkoa, akisema utaratibu wa kufanya usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi urejee na kila mmoja awajibike kikamilifu katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: