WAZIRI CHONGOLO ATATUA KERO SOKO MAZAO LA MAARUFU LA KAT MAGUVANI MAKAMBAKO
Автор: NJOMBE TV
Загружено: 2025-11-28
Просмотров: 2159
Описание:
WANAOJUA THAMANI YA MAENEO YAO HAWAKO TAYARI KUONO CHOCHOTE KIKIHARIBIWA- WAZIRI CHONGOLO
Makambako
Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo ametoa rai kwa watanzania na wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe kulinda kwa wivu mkubwa mali na miundombinu iliyopo kwenye maeneo yao ili kuto kuwa na sababu ya kurudi nyuma kimaendeleo kunakoweza kusababishwa na watu wachache.
Waziri Chongolo ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Makambako,ameeleza hayo alipokuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Maguvani pamoja na wafanyabiashara wa mali mbichi na mali kavu katika soko la Matema lililopo Maguvani Mjini Makambako.
"Hatuwezi kufika tunapotaka kama tutakaa kienyeji,ninyi mmesikia tarehe 29 kulitokea vurugu maeneo mbalimbali,hapa (kwenye soko) tunazungumzia kuweka mifuko 500 ya saruji ni kidogo? Tukichoma kesho patakuwa vilevile? Wenzetu wanaojua thamani ya eneo lao hawapo tayari kuona chochote kikiharibiwa"amesema Chongolo
Aidha Waziri Chongolo ametoa mifuko 500 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya wajasiriamali wadogo wanaouza mali mbichi,kavu pamoja na samaki katika mazingira magumu hususani kipindi cha mvua na Jua kali.
Awali akisoma taarifa ya soko hilo Katibu wa soko la Matema Yustina Sanga amesema soko hilo limeshika uchumi wa wanawake wapambanaji makambako hivyo wanaomba maboresho na mitaji ili kuinuka kiuchumi jambo ambalo Waziri Chongolo ameahidi kuendelea kufanyia kazi ili kuboresha mazingira na uchumi wa wajasiriamali hao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: