MJUMBE WA UN AFANYA ZIARA TANZANIA KUJADILI DEMOKRASIA
Автор: Baharia TV
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 194
Описание:
Parfait Onanga-Anyanga, Mwakilishi Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Umoja wa Afrika, amewasili Tanzania kwa ziara ya kikazi inayolenga kuimarisha demokrasia na utawala bora.
Ziara hiyo inafanyika baada ya matukio ya kisiasa ya Oktoba 29, 2025 yaliyosababisha changamoto za kiusalama katika baadhi ya maeneo ya nchi.
Akiwa Dar es Salaam, amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje Mahmoud Thabit Kombo na kuipongeza serikali kwa juhudi za kurejesha utulivu. Pia anatarajia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kama Chama Cha Mapinduzi, Chama cha Demokrasia na Maendeleo, ACT-Wazalendo na CHAUMMA kujadili njia za kuimarisha demokrasia, utawala bora na mshikamano wa kitaifa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: