Ni Salama Rohoni Mwangu | It Is Well With My Soul | Korir House
Автор: Korir House
Загружено: 2026-02-19
Просмотров: 332
Описание:
#music #gospelmusic #swahili NiSalamaRohoni
Nionapo amani kama shwari
Au nionapo shida;
Kwa hali zote umenijulisha
Ni salama rohoni mwangu
(Salama) salama rohoni,
ni salama rohoni mwangu X2
Ingawa shetani atanitesa
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu
(Salama) salama rohoni,
ni salama rohoni mwangu X2
Dhambi zangu zote, wala si nusu
Zimewekwa Msalabani
Wala sichukui laana yake
Ni salama rohoni mwangu
(Salama) salama rohoni,
ni salama rohoni mwangu X2
Ee Bwana himiza siku ya kuja
Panda itakapolia;
Utakaposhuka sitaogopa
Nisalama rohoni mwangu
(Salama) salama rohoni,
ni salama rohoni mwangu X2
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: