DC MAGOTI ACHARUKA VIBAYA "FUKUZA WOTE WAMEIFANYA KISARAWE SHAMBA LA BIBI"
Автор: J FIVE TV ONLINE
Загружено: 2024-12-01
Просмотров: 20646
Описание:
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti ameifuta baraza la ardhi la Kijiji cha Homboza kata ya Msimbu baada ya kubaini wajumbe wa baraza hilo kujihusisha na uuzaji holela wa ardhi bila kufuata sheria hali inayopelekea mgogoro mkubwa wa ardhi kijijini hapo.
Ametoa tamko hilo katika hafla ya kuwaapisha viongozi wapya wa serikali za vijiji na vitongoji, ambapo amewatahadharisha viongozi hao kujiepusha na uuzaji holela wa ardhi ya Kijiji badala yake wakatatue migogoro ya ardhi iliyopo katika maeneo yao, huku akiagiza wale wote waliotengeneza migogoro hiyo wawajibishwe.
DC Magoti ameonesha kuchukizwa na uuzaji holela wa ardhi ya vijiji wilayani humo na kuita kitendo hicho ni kama watu wameifanya wilaya hiyo kuwa shamba la bibi watu wajimilikisha hekari kwa hekari kinyume cha taratibu na sheria.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: