Maboresho ya Bandari ya Abiria Malindi kwa vitendo
Автор: Shirika la Bandari Zanzibar
Загружено: 2026-02-04
Просмотров: 53
Описание:
sekta ya bandari, Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) kwa kushirikiana na kampuni ya ZFDEVCO, linaendelea kutekeleza maboresho ya huduma katika Bandari ya Abiria Malindi kwa vitendo.
ZPC ilikabidhi rasmi majukumu ya uendeshaji wa Bandari ya Abiria Malindi kwa kampuni ya ZFDEVCO tarehe 01 Januari 2026, na tayari matokeo ya utekelezaji wa ahadi za maboresho yanaonekana wazi.
Katika hatua ya kuimarisha huduma kwa abiria, ZFDEVCO wamewasilisha na kuanza matumizi ya kifaa cha kisasa cha kubeba mizigo — 'Luggage Conveyor Belt' — ambacho tayari kimewasili na kinafanya kazi kikamilifu katika Bandari ya Abiria Malindi.
Mfumo huu umeboresha kwa kiasi kikubwa utaratibu wa upokeaji na uchukuaji wa mizigo, kwa kupunguza msongamano na kuongeza kasi pamoja na ufanisi wa huduma bandarini.
Kwa sasa, abiria wanapata huduma ya uchukuaji mizigo kwa utaratibu rahisi, wa haraka na salama zaidi, jambo linaloimarisha uzoefu wao wa usafiri na kuongeza hadhi ya huduma za bandari zetu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: