MSIBA MZITO: MUME ALIYEMUUA MKE, AKAJIREKODI 'VOICE NOTE' AKIELEZEA KWA UCHUNGU, UKWELI NI HUU..
Автор: Global TV Online
Загружено: 2022-08-02
Просмотров: 60601
Описание:
MSIBA MZITO: MUME ALIYEMUUA MKE, AKAJIREKODI 'VOICE NOTE' AKIELEZEA KWA UCHUNGU, UKWELI NI HUU..
Siku kadhaa zilizopita, picha ya mwanaume mmoja akiwa amembeba mtoto mdogo, pembeni yake kukiwa na mwanamke ilianza kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii ikisindikizwa na maneno kwamba mwanaume huyo alikuwa amemuua mwanamke anayeonekana kwenye picha hiyo kisha naye kujiua chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Muda mfupi baadaye, zikaanza kusambaa sauti za mwanaume aliyejirekodi ‘voice note’ kwa kutumia simu, akielezea jinsi alivyokuwa ametendewa unyanyasaji wa kimapenzi kwa mwanamke wake kumsaliti mara kwa mara.
Ikaelezwa kwamba sauti hizo, ni za mwanaume aliyekuwa akionekana kwenye picha ya awali na aliyekuwa akimlalamikia, ni mwanamke anayeonekana naye kwenye picha hiyo, gumzo likawa kubwa kwenye mitandao ya kijamii.
Kabla hilo halijatulia, ikaanza kusambaa sauti ya mwanamke aliyekuwa akizungumza kwenye simu na mwanaume, wakionesha kuwa wapenzi. Sauti hiyo ikaelezwa kwamba ni ya mwanamke anayeonekana kwenye ile picha na hapo alikuwa akizungumza na mwanaume mwingine tofauti na yule anayeonekana naye kwenye picha.
Baada ya kukusanya picha pamoja sauti hizo, Global TV iliamua kuchimba kwa undani kuhusu sakata hilo na kujua ni nini hasa kilichotokea mpaka kusababisha tukio hilo kuwa gumzo kubwa na ufuatao ni ufafanuzi wa kina wa tukio hilo.
Global TV imebaini kwamba ni kweli mwanaume anayeonekana kwenye picha hiyo, aliyetambuliwa kwa jina moja la Jerome ambaye kitaaluma alikuwa ni mwalimu wa sekondari japo hakuwa amepata ajira serikalini lakini amewahi kufundisha jijini Tanga, alimuua kwa kumnyonga mchumba wake kwa wivu wa kimapenzi kisha naye kujinyonga.
Tukio hilo limetokea Julai 25, 2022 katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Sumbawanga mjini mkoani Rukwa ambapo baada ya kufanya tukio hilo, alitoroka kuelekea Katavi ambapo naye alienda kujiua kwa kujinyonga.
⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8
⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx
⚫️ VISIT COMEDY PLAYLIST: https://www.youtube.com/playlist?list...
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE: ( +255 712 101 629), ( +255 784 888982)
⚫️ Email: [email protected] OR [email protected]
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ MICHEZO na BURUDANI: https://www.youtube.com/playlist?list...
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: http://bit.ly/mikasa_ya_kusisimua
⚫️ GLOBAL RADIO TV: http://bit.ly/255globalradio
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: http://bit.ly/exclusive_interviews
⚫️ Subscribe Global TV http://bit.ly/globaltvonline
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: