📍 HAI | DC NA MBUNGE WATULIZA WANANCHI WALIOAMUA KUCHUKUA HATUA!
Автор: TZA MEDIA HUB
Загружено: 2025-06-03
Просмотров: 12089
Описание:
Mkuu wa Wilaya ya Hai Hassan Bomboko, akiwa na Mbunge wa Hai Mhe. Saashisha Mafuwe, wameingilia kati na kutuliza hasira za wananchi waliokuwa wamekusanyika katika lango la shamba la Uduru Makoa, wakishinikiza kuondolewa kwa mwekezaji aliyedumu kwenye eneo hilo kwa zaidi ya miaka 20.
Wakiwa na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege, viongozi hao walifika kwenye eneo la tukio na kukutana na kundi la wananchi waliobeba mabango yenye ujumbe wa kutaka mwekezaji aondoke mara moja.
📌 Tukio hili limeibuka siku chache baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Moshi kutoa uamuzi kuwa chama cha ushirika cha UDURU MAKOA AMCOS kilifuata utaratibu wa kisheria kuvunja mkataba wa upangishaji shamba hilo kwa mujibu wa kifungu cha 16.2 cha mkataba wao wa mwaka 1999.
⚖ Mahakama imeeleza pia kuwa:
“Walalamikaji walikiuka masharti kadhaa ya msingi... hawakuwa na hiari ya kuchagua masharti ya kutekeleza na kuyaacha mengine.”
📣 Wananchi wanasisitiza kuwa sasa ni muda wa ardhi yao kuwanufaisha wenyewe, si wawekezaji wanaokiuka mikataba.
📰 Na @dixonbusagaga
📲 #CloudsDigitalUpdates
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: