Mbunge wa Malindi apinga kuondolewa kwa hazina ya NG-CDF
Автор: Coast Times Digital
Загружено: 2025-05-05
Просмотров: 1640
Описание:
Mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi, Amina Mnyazi amekashifu vikali hatua ya mahakama, kuagiza kuondolewa kwa hazina ya NG-CDF, kwa kile ilichosema uwepo wake ni kinyume cha sheria.
Kulingana na Mnyazi, kuwepo kwa fedha kwenye hazina hiyo, kumesaidia pakubwa kuboresha shughuli za elimu, kati ya wanafunzi wengi katika eneo bunge la Malindi na taifa la Kenya kwa jumla.
Akizungumza baada ya kutoa hundi za basari ya zaidi ya shilingi milioni 40, kwa wanafunzi zaidi ya elfu tano, ambao wazazi wao ni wakaazi wa eneo hili la Malindi, amesema kuwa kuondolewa kwa fedha hizo, kutasababisha wanaf.unzi wa familia zisizo na uwezo mzuri wa kifedha kukosa kusoma.
Kauli yake imepigwa jeki na baadhi YA wakazi Wa eneo Bunge la malindi ambao wamesema kuwa mfumo wa ugavi wa basari unaotumika kwa sasa, umesaidia pakubwa wanafunzi wote kupata fedha hizo na hata kusalia shule ili kuboresha matokeo yao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: