SERIKALI YACHOCHEA KILIMO TANGANYIKA, DC BUSWELU AONGOZA MAKABIDHIANO YA ZANA.
Автор: HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA
Загружено: 2026-02-06
Просмотров: 139
Описание:
SERIKALI YACHOCHEA KILIMO TANGANYIKA, DC BUSWELU AONGOZA MAKABIDHIANO YA ZANA.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu, leo amekabidhi jumla ya trekta za mikono 16 (Power Tiler) kwa wakulima wa Kata nne za Katuma, Mnyagala, Karema na Sibwesa. Zana hizo zimetolewa na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao wilayani humo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Buswelu ameishauri Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kupitia Mwenyekiti wake, Mhe. Hamadi Mapengo, na Mkurugenzi Mtendaji, kutenga bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 kwa ajili ya kununua zana zaidi za kilimo. Alisisitiza kuwa hatua hiyo itachochea kasi ya kilimo na kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.
Katika hotuba yake, DC Buswelu amewataka viongozi wa Halmashauri kuiga mfano wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza kwa kupeleka zana hizo kama mwanzo wa mabadiliko. Amesema kuwa hata kama halmashauri itashindwa kuongeza idadi kubwa ya Power Tiler, ni vyema ikaongeza angalau moja zaidi ili mapato ya ndani yaweze kutumika kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Mapengo ameeleza kuwa Kata zilizopokea zana hizo ni zile zenye shughuli kubwa za kilimo, na akasisitiza kuwa mashine hizo zitakuwa zinatumika pia katika kata nyingine kulingana na mahitaji. Wanufaika wa zana hizo wametoa shukrani kwa Serikali na Rais Samia kwa kuwapatia zana za kisasa, huku wakiahidi kuvitunza vifaa hivyo kwa kuwa ni sehemu ya ajira na kipato chao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: