Ofisi ya Taifa ya Takwimu yawa mfano wa utendaji kazi bora, RC Malima awapongeza
Автор: RS MOROGORO
Загружено: 2025-12-19
Просмотров: 38
Описание:
Ofisi ya Taifa ya Takwimu yawa mfano wa utendaji kazi bora, RC Malima awapongeza
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa utekelezaji wa sheria na kanuni zinazounda mabaraza ya wafanyakazi pamoja na namna inavyofanya kazi na jamii, hivyo kuwa mfano bora wa kuigwa na taasisi nyingine.
Mhe. Malima ametoa pongezi hizo Disemba 19, 2025, wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu uliofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Mkoa wa Morogoro.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema NBS inafanya kazi ya kutoa huduma za takwimu kwa jamii, hivyo ameipongeza kwa juhudi inazozifanya taasisi hiyo kuhakikisha jamii inapata takwimu sahihi kwa wakati muafaka. Aidha, amesema NBS imeendelea kuzingatia sheria za mabaraza ya wafanyakazi, kwani mabaraza hayo husaidia watumishi kutoa changamoto zao na kupata namna bora ya kuzitatua.
“Namna mnavyofanya kazi na jamii, NBS mmekuwa mfano siku zote, na mimi nawatakia heri muendelee kuwa mfano,” amesisitiza Mhe. Adam Malima.
Aidha, Mhe. Malima amesema suala la mabaraza ya wafanyakazi katika sehemu za kazi si hisani, bali ni kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa na Serikali.
“...Mabaraza ya wafanyakazi kwenye sehemu za kazi si hisani...,” amesisitiza Mhe. Adam Malima.
Kwa upande wake, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda, amewataka watumishi wa takwimu kutumia baraza hilo kuhakikisha wanatoa maoni, ushauri na changamoto wanazokumbana nazo, na kutojiwekea changamoto moyoni kwani jambo hilo hupelekea kudorora kwa utendaji kazi.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Dkt. Amina Msengwa, amesema Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeendelea na utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango Kabambe wa Kuboresha Takwimu Nchini, ambapo inawajengea uwezo watumishi wa takwimu nchini, kuboresha ukusanyaji na usambazaji wa takwimu, jambo litakalopelekea upatikanaji wa takwimu bora.
Mwisho.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: