Ndugu Wa Mama Aliyefungwa Jela Miaka 22 Kisa Nyama ya Swala Wafunguka | Wanatia Huruma Sana
Автор: Focus TV Tanzania
Загружено: 2023-11-10
Просмотров: 3119
Описание:
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa ilimuhukumu kifungo cha miaka 22 Jela, Maria Ngoda Mkazi wa Mtaa wa Zizi la ng'ombe uliopo katika Manispaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kumkuta na hatia ya kukutwa na ndoo yenye vipande 12 vya nyama ya swala kinyume na sheria.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha kuwa ni Kweli Maria alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo ya swala yenye vipande 12 ndani yake vyenye thamaj ya Tsh. laki tisa ambapo ushahidi uliotolewa ulisema kuwa siku ya tukio Maria alikutwa na ndoo hiyo yenye vipande 12 vya nyama ya swala aliyokuwa akiiuza karibu na nyumba yake na hivyo nyama hiyo ikafikishwa kwa Mtambuzi na kubaini ni kweli ilikuwa ya Swala na baada ya tathmini gharama yake ikafika Tsh. laki tisa.
Kwa upande wake Mtuhumiwa wakati akijitetea alikiri ni kweli alikutwa na ndoo hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na Mtu aliyemtambua kwa jina la Fute na awali hakujua ni nyama ya nini ndani yake.
Hata hivyo hukumu hii imeibua hisia za watu wengi, Wadau na Wanasheria kutokana na jinsi shauri lilivyoendeshwa kwani Mtuhumiwa hakupata uwakilishi wa kumtetea kipindi chote cha kesi yake hivyo baadhi ya wadau na Mawakili wamejitolea kukata rufaa na kumsaidia Mtuhumiwa katika kesi hii ikiwemo Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) chini ya Mwenyekiti wake Mary Chatanda ilisema imesikitishwa na uamuzi huo na itaona jinsi ya kumsaidia Mwanamke huyo kukata rufaa na kumsaidia kupata uwakilishi mzuri ili aweze kupata haki yake.
Focus Digito TV imefika mpaka Zizi la Ng'ombe alipokuwa anaishi Mtuhumiwa kujionea maisha halisi na kupata taarifa zaidi kwa kufanya mahojiano na Ndugu zake akiwemo Dada wa Mtuhumiwa na Mtoto wa Mtuhumiwa.
Subscribe (Focus Digito TV) ili usipitwe na Video kama hii.
Focus Digito TV inakupa Maudhui Mazuri yanayohusu mitindo ya maisha na Burudani.
Focus Digito TV is here to provide you with contents about Lifestyles and Entertainments.
#FocusDigitoTV
..................
Tufuatilie Zaidi:
INSTAGRAM: / focusdigitotv
TIKTOK: https://www.tiktok.com/focusdigitotv/
TWITTER: / focusdigito
FACEBOOK: / focusdigitotv
YouTube: https://www.youtube/@focusdigitotv
We Post InfoEduTainment Videos conveying messages about Lifestyles and Entertainments, justfor You to Watch and Enjoy.
We Love You | Tunakupenda
Regards
Team FocusDigitoTV
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: