Huyu hapa Mazurui, aibuka na Mapya kuhusu SMZ
Автор: MD TV ZANZIBAR
Загружено: 2024-08-27
Просмотров: 71
Описание:
#MDtvznz #Micheweni_Digital_Tv #Enjoy_Digital_Content
Waziri wa Afya Mhe. Nassor Ahmed #Mazurui amesema Serikali imeweka mikakati madhubuti katika kukabiliana na majanga mbali mbali na kutokomeza kabisa ulemavu na vifo vinavyoweza kuepukika.
Mhe. Mazrui amesema kuwa uwepo wa mifumo Imara na endelevu ya kutoa huduma ya tiba ya dharura na wagonjwa mahtuti kwa wakati kutapunguza vifo vya mama wajawazito na watoto na hata majanga yatokanayo na ajali mbali mbali ambayo yanaendelea kugharimu maisha ya wananchi wengi.
Amesema licha ya uhaba wa madaktari bingwa wanaoshuhulikia utoaji wa huduma za dharura na wagonjwa mahtuti bado jitihada ya makusudi zinahitajika kutoka katika kitengo cha Imajensi na vitengo vyengine vya tiba kwa kufanya kazi kwa kushirikiana katika kutoa matibabu ya haraka kwa wananchi ili kuokoa maisha ya wananchi wengi.
Tembelea Blog yetu
https://michewenidigitaltv.blogspot.com/
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: